Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Kyela Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akielekea Ukumbini kwa ajili ya kwenda kutoa mhadhara wa kuchochea utoaji wa maoni katika kuijadili rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Baraza la Kuijadili Rasimu ya Katiba lililokuwa likifanywa na Taasisi ya Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu Nchini (TAHLISO). Kulia kabisa ni Ndg. Silasi Malima - Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO, anayefuatia wa pili kulia ni Ndg. Amon Chakushemeire - Mwenyekiti wa TAHLISO, Upande wa Kushoto ni Ndg. Donati Primi Salla - Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO, na wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, na Nyuma yake Ni Ndg. Haji Rozzo - Naibu Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Dkt. Norman Msigalla (katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Baraza la Katiba la TAHLISO baada ya kufungua rasmi Baraza la Katiba la TAHLISO mnamo tarehe 02/08/2013. Upande wa kulia ni Mhe. Amon Chakushemeire - Mwenyekiti wa TAHLISO, na Ndg. Theofan Theonest - Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Wa Kwanza Upande wa Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, na Mhe. Silasi Malima - Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO. Wengine ni Makamishna na Viongozi wa juu wa TAHLISO.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fredrick Sumaye (katikati) akielekea ukumbini kwa ajili ya kwenda kufunga mkutano wa Baraza la Katiba la TAHLISO lililofanyika mnamo tarehe 02 -03 Agosti 2013 katika Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Wengine kwa upande wa kulia ni Ndg. Amon Chakushemeire - Mwenyekiti wa TAHLISO, na wa pili kulia ni Ndg . Silasi Malima - Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO. Upande wa kushoto ni Ndg. Donati Primi Salla - Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO.
No comments:
Post a Comment