Wajumbe wa Taasisi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) walikutana Mnamo tarehe 02 na 03 Mwezi Agosti 2013 kujadili rasimu mpya ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mjadala huo ulizinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt. Norman Msigallah pamoja na kukolezwa na Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Kyela ili kuwafanya wasomi wapate hamasa ya kujadili rasimu hiyo kwa kina zaidi.
Pamoja na Mambo Mengine Mjadala huo uliendeshwa vizuri ambapo Asilimia 86.5 ya wajumbe wote walioalikwa kwenye Mkutano huo walihudhuria.
Kwa Upande Mwingine Mwenyekiti wa TAHLISO Ndugu Amon Chakushemeire alisema kuwa TAHLISO kama moja ya taasisi ya wasomi wa Vyuo vya Elimu ya Juu iliona kuwa ni busara kuijadili Rasimu ya Katiba hiyo ili kuandaa mazingira mazuri ya Ustawi wa Tanzania ya Kesho.
Baada ya kumalizika kwa mjadala wa Rasimu hiyo, Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fredrick Sumaye.
No comments:
Post a Comment