Welcome!

Tanzania Higher Learning Institutions Students' Organization also known by acronym as "TAHLISO" is a National Union of Students from all Higher Learning Institutions residing in both Tanzania Mainland and Tanzania Islands of Zanzibar.
The Higher Learning Institutions in Tanzania are;
1. Universities.
2. University Colleges.
3. University Centers.
4. Non Degree Institutions which offers the Degree programs from first degree and above.
This is subject to Universities Act No. 7 of 2005 and the National Council for Technical Education of 1997 of the United Republic of Tanzania.
The Secretariat of TAHLISO would like to welcome you is this site and take a time to know the functions of TAHLISO in Tanzania.

Mr. Donati Salla
The Executive Secretary General.

Saturday, 24 August 2013

TAARIFA RASMI YA TAHLISO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MKUTANO WA BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU ULIOFANYIKA AGOSTI 18, 2013 MKOANI MOROGORO.

Utangulizi.
Ndugu Wanahabari;
Mnamo Jumatatu ya juma hili yaani siku ya Agusti 19, 2013 gazeti la Majira toleo Na: 7166, gazeti la Jambo leo toleo Na: 1440, na gazeti la Mwananchi toleo Na: 4796 na vyombo vingine vya habari viliripoti juu ya Mkutano wa baadhi ya Viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo vya elimu ya juu hapa nchini uliofanyika mkoani Morogoro. Mkutano huo uliwakutanisha baadhi ya Marais wa Serikali za Wanafunzi, Makamu wa Rais wa Serikali za wanafunzi,  Maspika wa mabunge ya Serikali za Wanafunzi, na Viongozi waandamizi kutoka kwenye serikali mbambali za wanafunzi ambapo inasemekana kuwa mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya kupambana na maadui watatu ambao ni Ujinga, Maradhi, na Umaskini, inayofakamika kama FPID ambapo taasisi hiyo ina makao yake makuu hapa Jijini Dar es Salaam.

Kwa Mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mkutano huo uliofanyika morogoro ulijadili masuala ya utouti wa kipato kati ya watanzania, ubora wa elimu hasa maeneo ya vijijini, na fursa za ajira. Lakini kubwa lililoibuka katika mkutano huu na kuchukua uzito mkubwa wa Mkutano wenyewe ni suala la ‘ni nani awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mnamo Mwaka 2015’

Taarifa Rasmi Kutoka TAHLISO.
Taasisi ya Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu imesikitishwa sana na inalaani vikali matukio  yaliyojitokeza katika Mkutano huo kwani ni kinyume na maadili ya Elimu ya Juu hapa nchini. Watu wengi wamehusisha Mkutano huo na taasisi yetu ya TAHLISO kwamba TAHLISO ndiyo iliyoandaa Mkutano huo jambo ambalo sivyo.
Pamoja na hayo TAHLISO inaarifu mambo yafuatayo kwa Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba;-

  •   Mkutano Ulioitishwa Mkoani Morogoro ni batili na hautambuliki kwa mujibu wa sheria Na. 07 ya vyuo vikuu ya Mwaka 2005, sheria ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002 pamoja na Katiba ya TAHLISO. 
  •  Shughuli za serikali za wanafunzi katika vyuo vya elimu ya juu ni kushuhulika na  masuala ya wanafunzi na ubora wa taaluma itolewayo katika chuo husika na masuala mengine ya kitaifa lakini si kwa ushabiki wa kisiasa au kutetea kundi au maslahi ya watu fulani.
  • Ni Jukumu la vyama vya siasa vilivyosajiliwa na kutambulika kiserikali kukaa na kuchagua au kuteua wajumbe wanaogombea nafasi mbalimbali za kisiasa iwe katika chama, serikali au vinginevyo lakini hilo siyo jukumu la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.
  • Vikao vyote vinavyohusu mjumuiko wa serikali za wanafunzi vinapaswa kuitishwa na kuratibiwa na TAHLISO na siyo taasisi nyingine yeyote.
 Hatua zilizochukuliwa na TAHLISO kuhusiana na yaliyotokana na Mkutano wa     baadhi wa Viongozi wa Serikali za Wanafunzi Mkoani Morogoro.
  • TAHLISO inatoa onyo kali kwa viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambao walishiriki kwenye Mkutano huo wa Morogoro kwamba wasirudie tena kufanya hivyo na vinara wa wanafunzi ambao walikuwa mstari wa mbele kuchochea masuala haya ya kisiasa bila ya kufuata utaratibu watawajibishwa ipasavyo.
  •  Ni marufuku kwa wanafunzi au makundi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kuendesha harakati za siasa kwa kutumia jina la chuo, vyuo, au taasisi yoyote inayoshughulika na masuala la elimu ya juu hapa nchini.
  •   TAHLISO itawaandikia barua Waadili wote wa wanafunzi (Deans of Students) wa vyuo vya elimu ya juu na kuwapatia hadidu za rejea kuhusu utaratibu wa kubaini vikao halali na visivyo halali ili waweze kuratibu vyema ruhusa zitolewazo kwa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kwa ajili ya kuhudhuria mikutano mbalimbali ambayo ipo nje na taratibu za chuo husika na inayohusiana na masuala ya wanafunzi kitaifa au vinginevyo. 
  •   Kwa onyo hili la awali Viongozi wa Serikali  za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu watakaokiuka taratibu zilizoainishwa hapa watawajibishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za adhabu zilizopo kwenye chuo husika.
  Mwisho.
 TAHLISO inawakumbusha wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini kwamba, jukumu lao ni kusoma na kujifunza taaluma zao kwa taratibu zilizoanishwa na chuo husika. Hicho ndicho kilichowapeleka chuoni kwa hiyo wafanye masomo kwanza, na chama chao ni taaluma, kisha siasa watafanya baadaye.

Imetolewa na Ndg. Donati Primi Salla
Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO

MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE BARAZA LA KATIBA LA TAHLISO LILILOFANYIKA TAREHE 02 - 03 AGOSTI 2013 KATIKA CHUO KIKUU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA


Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Kyela Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akielekea Ukumbini kwa ajili ya kwenda kutoa mhadhara wa kuchochea utoaji wa maoni katika kuijadili rasimu ya kwanza ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Baraza la Kuijadili Rasimu ya Katiba lililokuwa likifanywa na Taasisi ya Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu Nchini (TAHLISO). Kulia kabisa ni Ndg. Silasi Malima - Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO, anayefuatia wa pili kulia ni Ndg. Amon Chakushemeire - Mwenyekiti wa TAHLISO, Upande wa Kushoto ni Ndg. Donati Primi Salla - Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO, na wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, na Nyuma yake Ni Ndg. Haji Rozzo - Naibu Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Dkt. Norman Msigalla (katikati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Baraza la Katiba la TAHLISO baada ya kufungua rasmi Baraza la Katiba la TAHLISO mnamo tarehe 02/08/2013. Upande wa kulia ni Mhe. Amon Chakushemeire - Mwenyekiti wa TAHLISO, na Ndg. Theofan Theonest - Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Wa Kwanza Upande wa Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, na Mhe. Silasi Malima - Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO. Wengine ni Makamishna na Viongozi wa juu wa TAHLISO.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fredrick Sumaye (katikati) akielekea ukumbini kwa ajili ya kwenda kufunga mkutano wa Baraza la Katiba la TAHLISO lililofanyika mnamo tarehe 02 -03 Agosti 2013 katika Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Wengine kwa upande wa kulia ni Ndg. Amon Chakushemeire - Mwenyekiti wa TAHLISO,  na wa pili kulia ni Ndg . Silasi Malima - Mwenyekiti wa Seneti ya TAHLISO. Upande wa kushoto ni Ndg. Donati Primi Salla - Katibu Mkuu Mtendaji wa TAHLISO.

Friday, 16 August 2013

Baraza la Kujadili Rasimu ya Katiba Mpya ya Tanzania Lafana!

        Wajumbe wa Taasisi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) walikutana Mnamo tarehe 02 na 03 Mwezi Agosti 2013 kujadili rasimu mpya ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Mjadala huo ulizinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt. Norman Msigallah pamoja na kukolezwa na Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Kyela ili kuwafanya wasomi wapate hamasa ya kujadili rasimu hiyo kwa kina zaidi. 
Pamoja na Mambo Mengine Mjadala huo uliendeshwa vizuri ambapo Asilimia 86.5 ya wajumbe wote walioalikwa kwenye Mkutano huo walihudhuria.
Kwa Upande Mwingine Mwenyekiti wa TAHLISO Ndugu Amon Chakushemeire alisema kuwa TAHLISO kama moja ya taasisi ya wasomi wa Vyuo vya Elimu ya Juu iliona kuwa ni busara kuijadili Rasimu ya Katiba hiyo ili kuandaa mazingira mazuri ya Ustawi wa Tanzania ya Kesho.
Baada ya kumalizika kwa mjadala wa Rasimu hiyo, Mkutano huo ulifungwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Fredrick Sumaye.